NCC YASHIRIKI KONGAMANO LA MWAKA LA AQRB JIJINI AR...

NCC YASHIRIKI KONGAMANO LA MWAKA LA AQRB JIJINI ARUSHA

22 Oct, 2026
NCC YASHIRIKI KONGAMANO LA MWAKA LA AQRB JIJINI ARUSHA

Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) limeshiriki Kongamano la Mwaka la Bodi ya Usajili wa Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) 2026, lililoanza leo, Oktoba 21, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NCC, Mha. Dkt. Matiko Mturi, ameshiriki katika kongamano hilo linalowakutanisha wataalamu na wadau wa tasnia ya ujenzi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, kujenga mahusiano ya kitaalamu na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kongamano hilo limefunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Eng. Godfrey Kasekenya, na linatarajiwa kuendelea hadi Ijumaa, Oktoba 23, 2026.

Kupitia kongamano hilo, NCC inaendelea kushirikiana na wadau wa tasnia ya ujenzi katika kubadilishana maarifa, uzoefu na mawazo yatakayochangia kuboresha utendaji wa sekta hiyo.

Ushiriki huu pia unatoa fursa ya kujadili changamoto na mbinu bora za kitaalamu, kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi na wadau, na kuchochea maendeleo endelevu ya tasnia ya ujenzi nchini.