Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Bei ya Price Indices ni Tsh. 500,000.00
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ni taasisi ya serikali iliyoanzishwa mwaka 1979 kupitia Sheria ya Bunge Na. 20 na kuanza rasmi kutekeleza majukumu yake tarehe 17 Agosti 1981 kupitia Tangazo la Serikali Na. 95 la mwaka 1981. Mwaka 2007, sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho kupitia Sheria ya Bunge Na. 25 ya mwaka 2007, kama ilivyorejewa katika Toleo Lililorekebishwa la Sura ya 162 la mwaka 2008 na imejumuishwa katika Toleo lililorekebishwa la Sheria (Revised Edition) la mwaka 2023, linalojulikana kama National Construction Council Act, CAP 162, R.E. 2023.
Huduma zetu zinahusisha ukaguzi wa miradi na mifumo mbalimbali.
NCC hufanya ukaguzi wa kiufundi wa:
Majengo
Barabara
Madaraja
Miradi ya maji
Miundombinu mingine ya ujenzi
Mashine
Mitambo
NCC hufanya ukaguzi wa kiufundi wa:
Majengo
Barabara
Madaraja
Miradi ya maji
Miundombinu mingine ya ujenzi
Mashine
Mitambo
Kaguzi za kiufundi zinaweza kufanywa katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi, kulingana na mahitaji ya mradi husika au maamuzi ya mtekelezaji wa mradi yanayotokana na tathmini ya vihatarishi (risk assessment).
NCC hutoa huduma za ushauri wa kitaalamu katika maeneo mbalimbali yanayohusiana na utekelezaji wa miradi ya ujenzi na shughuli nyingine zinazohusiana na sekta ya ujenzi. Ushauri huu unalenga kusaidia wateja kufanya maamuzi sahihi, kuboresha usimamizi wa miradi, kudhibiti vihatarishi na kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ufanisi, ubora na thamani inayostahili.
Wadau wote wa ujenzi wanaweza kuomba ushauri kutoka baraza la taifa la ujenzi (NCC).
Njedengwa Jengo la Mfuko wa Barabara (Roads Fund Board Building)