Majukumu

Majukumu

  1. Kuhamasisha na kuweka mikakati ya kukuza, kuendeleza na kupanua Sekta ya Ujenzi nchini Tanzania husasan kwa kujenga uwezo na ushindani wa wazawa ili waweze kushindana na kutekeleza miradi kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi;
  2. Kushauri Serikali juu ya maendeleo ya Sekta ya Ujenzi nchini na kuandaa mapendekezo ya utekelezaji wa ushauri huo;
  3. Kutoa ushauri na msaada wa kitaalamu kwa wadau wa Sekta ya Ujenzi nchini kuhusu mambo yanayohusiana na sekta ya ujenzi;
  4. Kuratibu na kuendeleza mafunzo bora kwa wote wanaojihusisha au wanaotarajia kujihusisha na shughuli za ujenzi na shughuli nyingine katika Sekta ya Ujenzi nchini;
  5. Kufanya, kuhimiza na kuratibu utafiti katika shughuli zote za Sekta ya Ujenzi;
  6. Kuhamasisha, kukusanya, kuchakata na kuchapisha taarifa mbalimbali zinazohusu Sekta ya Ujenzi;
  7. Kuhamasisha na kufuatilia uandaaji na utumiaji wa viwango vya ubora, kanuni na miongozo mbalimbali inayohusiana na shughuli za Sekta ya Ujenzi nchini;
  8. Kuhamasisha, kushawishi, kubuni na kutumia teknolojia bora na mbinu bora za utendaji katika Sekta ya Ujenzi nchini;
  9. Kuhamasisha na kuanzisha majukwaa ili kuratibu shughuli za wadau wa Sekta ya Ujenzi na kuwezesha kushirikiana na kujadiliana katika masuala yanayohusu maendeleo ya Sekta ya Ujenzi nchini;
  10. Kufuatilia, kutathmini na kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za Sekta ya Ujenzi nchini;
  11. Kutafuta na kusimamia fedha za mafunzo ya wataalum na mafundi katika Sekta ya Ujenzi;
  12. Kuhamasisha ubora katika sekta ya ujenzi, ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa kiufundi wa miradi ya ujenzi;
  13. Kuhamasisha mbinu za ujenzi zenye kuzingatia uhifadhi endelevu wa mazingira pamoja na afya na usalama wa kazi katika shughuli za ujenzi;
  14. Kuhamasisha kuuza nje bidhaa na huduma za sekta ya ujenzi; na
  15. Kuratibu na kuwezesha utatuzi wa migogoro inayotokea katika miradi ya ujenzi kwa ufanisi.