


Naibu Waziri Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mha. Geofrey Mwakasenga kuhusu NCC alipotembelea banda la Baraza wakati maonesho ya taasisi za Wizara ya Ujenzi katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Bw. Ludovick J. Nduhiye akisaini kitabu cha wageni wakati wa maonesho ya taasisi za Wizara ya Ujenzi yaliyofanyika katika viunga vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, alilipongeza Baraza kwa kazi nzuri linazozifanya za kuendeleza sekta ya ujenzi nchini.

Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) wakishiriki katika Maadhimisho ya Sukukuu ya Wafanyakazi Dunia 'Mei Mosi' katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) wakishiriki katika Maadhimisho ya Sukukuu ya Wafanyakazi Dunia 'Mei Mosi' katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu Uwezeshaji wa Wakandarasi Wazawa kupewa kipaumbele kushiriki katika miradi ya ujenzi nchini na Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Mha. Dkt. Matiko Mturi (wa tano kulia) akiendesha mdahalo juu ya maendeleo ya kazi za kamati wakati wa hafla ya kuangazia mafanikio ya miaka mitatu madarakani ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika katika Ukumbi wa Jen. Venance Mabeyo Jijini Dodoma.

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa akifuatilia mdahalo juu ya maendeleo ya kazi za kamati wakati wa hafla ya kuangazia mafanikio ya miaka mitatu madarakani ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika katika Ukumbi wa Jen. Venance Mabeyo Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu Uwezeshaji wa Wakandarasi Wazawa kupewa kipaumbele kushiriki katika miradi ya ujenzi nchini na Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Mha. Dkt. Matiko Mturi akiendesha mdahalo juu ya maendeleo ya kazi za kamati wakati wa hafla ya kuangazia mafanikio ya miaka mitatu madarakani ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyofanyika katika Ukumbi wa Jen. Venance Mabeyo Jijini Dodoma.

NCC inatekeleza kwa vitendo sera ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza(NCD)

Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) wakifanya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya zao jana katika viunga vya Bodi ya Mfuko wa Barabara, Njedengwa jijini Dodoma.

Wajumbe wa Baraza la NCC wakishiriki katika Mkutano wa 105 wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa NCC mjini Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NCC Mha. Dkt. Matiko Mturi akiwasilisha taarifa kwa Baraza la NCC wakati wa Mkutano wa 105 wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa NCC jijini Dodoma.

Wajumbe wa Baraza la NCC wakishiriki katika Mkutano wa 105 wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa NCC, mjini Dodoma.

Wajumbe wa Baraza la NCC wakishiriki katika Mkutano wa 105 wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa NCC jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Baraza la NCC Dkt. Fatma Mohamed akiendesha Mkutano wa 105 wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa NCC, jijini Dodoma.

Mshiriki wa wa mafunzo yaliyoendeshwa na NCC Mha.Debora M.Kanyika kutoka RUWASA akipokea cheti kutoka kwa Mkufunzi wa NCC Wakili/Mkadiriaji Majenzi Elias Kissamo baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo yalioendeshwa na NCC wakimsikiliza Mha. Devota Kafuku wa TANROADS walipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Magufuli jijini Mwanza

Washiriki wa mafunzo yalioendeshwa na NCC wakifuatilia kwa karibu uwasilishwaji wa mada katika Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza

Mwenyekiti wa Kamati ya Kuandaa Mkakati wa Kuwawezesha Makandarasi Wazawa kushiriki katika miradi ya Serikali Mha. Dkt Matiko Mturi akiwasilisha andiko hilo leo jijini Dodoma. Dkt. Mturi pia ni Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ambayo imepewa jukumu la kuratibu kamati hiyo

Sehemu ya wajumbe na washiriki wa mkutano wakifuatilia mjadala baada ya wasilisho la Kamati inayoandaa Mkakati wa Kuwawezesha Makandarasi Wazawa kushiriki katika miradi ya Serikali. NCC ilipewa jukumu na Serikali la kuratibu kamati hiyo.

Mwenyekiti wa Baraza la NCC Dkt. Fatma Mohamed akichangia katika mjadala baada ya wasilisho la Kamati inayoandaa Mkakati wa Kuwawezesha Makandarasi Wazawa kushiriki katika miradi ya Serikali. NCC ilipewa jukumu na Serikali la kuratibu kamati hiyo

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kupokea wasilisho la Kamati inayoandaa Mkakati wa Kuwawezesha Makandarasi Wazawa kushiriki katika miradi ya Serikali. Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Mha. Dkt Matiko Mturi amewasilisha andiko hilo leo 09.02.2024 jijini Dodoma.

Washiriki wa Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali na Makandarasi na Washauri Elekezi wa Ndani wakifuatilia kwa makini wasilisho la Mha. Dkt. Matiko Mturi Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) na Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu mikakati ya kuongeza ushiriki wa wazawa (makandarasi na washauri elekezi) katika miradi ya ujenzi nchini. Mkutano huo ulifanyika tarehe 21 Novemba 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu Uwezeshaji wa Wakandarasi Wazawa kupewa kipaumbele kushiriki katika miradi ya ujenzi nchi na Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Mha. Dkt. Matiko Mturi akitoa taarifa ya kamati hiyo wakati wa Mkutano wa Mashauriano kati ya Serikali na Makandarasi na Washauri Elekezi wa ndani kwa ajili ya kujadili nafasi yao katika utekelezaji wa miradi uliofanyika 21 Novemba 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Habari Mpya
-
NCC yashiriki maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
WATUMISHI wanawake wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), wameungana na wanawake wenzao duniani kusherehekea siku yao, iliyolenga kusisitiza haki, usawa na uwezeshaji kwa wasichana na wanawake.
Mar 10,2025 Soma zaidi -
NAIBU WAZIRI UJENZI AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA BARAZA LA TAIFA LA UJENZI (NCC)
Oct 24,2024 Soma zaidi -
Dk Msonde atembelea NCC
Sep 30,2024 Soma zaidi
Soma Habari zaidi