Kupitia mafunzo malumu ya usimamizi wa mikataba ya manunuzi ya ujenzi
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) imeendelea kuimarisha sekta ya ujenzi nchini kwa kutoa mafunzo yanayolenga kujenga uwezo kwa wadau mbalimbali. Mbali na mafunzo ya kawaida yanayotangazwa kwa umma, NCC pia hutoa mafunzo maalumu yanayoandaliwa kulingana na mahitaji ya taasisi husika, kwa kuzingatia maeneo yenye changamoto au yanayohitaji kuongeza ufanisi katika sekta ya ujenzi.
Katika kutekeleza jukumu hilo, NCC imetoa Mafunzo Maalumu ya Usimamizi wa mikataba ya manunuzi ya ujenzi kwa Ofisi ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Akizungumza jijini Morogoro wakati wa mafunzo hayo, Mhandisi,Dkt.Paul Busondole ambae ni mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo amesema, mafunzo hayo yamelenga kuhakikisha wanasheria hao kutoka NSSF wanazingatia ubora wa mikataba ya ujenzi, gharama zinakuwa halisi na miradi inakamilika kwa wakati na pia kupunguza migogoro wakati wa utekelezaji wa miradi.
" Faida kubwa ya mafunzo haya ni kwamba Taasisi za umma zitaweza kupata thamani ya fedha wanazolipia kwa kuhakikisha ubora unazingatiwa, gharama zinakuwa halisi na miradi inakamilika kwa wakati, lakini mafunzo haya pia yanasaidia kupunguza migogoro na migongano wakati wa utekelezaji wa miradi.aidha itawezesha washiriki kushauri taasisi nyingine kuweza kutumia rasilimali zetu kwa ubora na kwa wakati itakayosaidia kukuza maendeleo ya nchi kuelekea dira ya taifa ya maendeleo ya 2050” amesema
Kwa upande wa washiriki,Mwanasheria kutoka NSSF, Grace Thomas Mushi, amesema mafunzo haya ni muhimu kwa wanasheria kwa sababu ili kuhakikisha miradi inakamilika vizuri lazima kuwepo na usimamizi mzuri wa mikataba ya ujenzi, wakati wa uandaaji na pia wakati wa upekuzi wa mikataba hiyo ili kupunguza migogoro inayokwamisha utekelezaji wa miradi.
“Mafunzo haya ni muhimu sana kwa sababu unapoanza mafunzo na unapomaliza unajiona kabisa umetoka tofauti umepata kitu kikubwa kama vile kujua namna sahihi ya kuandaa mikataba yetu, kuikagua lakini pia kusimamia miradi’’amesema
Naye,Mwanasheria Daudi Maneno kutoka NSSF ameongeza kuwa mafunzo yanayotolewa na NCC yana mchango katika kukuza maendeleo ya nchi kwa sababu yanaandaa wataalamu watakaotekeleza miradi kwa weledi hivyo kukuza sekta ya ujenzi itakayochochea maendeleo ya nchi kwa ujumla.
“Mafunzo yanayotolewa na NCC yana mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi kwa sababu sekta ya ujenzi ndio driving sector ya nchi,kwahiyo NCC inasaidia kuandaa wajenzi wazuri wenye utaalamu watakaoweza kukamilisha miradi kwa wakati hivyo kukuza Uchumi wa nchi”amesema
Kupitia Mafunzo haya, NCC inaendelea kutoa wito kwa taasisi za umma na binafsi kutumia fursa ya kuomba mafunzo maalumu yanayolenga maeneo wanayohitaji kujengewa uwezo. Hatua hii inaendelea kuchangia kuimarisha rasilimali watu, kuongeza ufanisi katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya ujenzi, na kukuza ubora wa sekta ya ujenzi nchini.
Sekta ya Ujenzi ni moja ya nguzo muhimu za utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maend...
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Baraza la Taifa la Ujenzi (N...
Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, amewataka wakandarasi nchini kutekeleza m...
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) limesema uwezekano wa migogoro ya kib...
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe...