Usuluhishi wa Migogoro

Tangu mwaka 1982 Baraza limekuwa likiratibu usuluhishi wa migogoro ya ujenzi. Baraza lina orodha ya wasuluhishi wa migogoro ya ujenzi ambao husajiliwa kutokana na sifa zao, na hawa wanaweza kutumiwa na wateja kwa kuchagua wenyewe.Aidha, utatuzi wa migogoro hufuata miongozo ya usuluhishi ambayo huchapishwa na Baraza.