Uratibu wa Sekta ya Ujenzi
Sera na Mikakati
Baraza limehusika katika uratibu na uundaji wa sera na mikakati mbalimbali kwa ajili ya sekta ya ujenzi kama ifuatavyo:
- Mkakati wa Maendeleo ya Sekta ya Ujenzi wa mwaka 1991
- Sera ya Sekta ya Ujenzi ya mwaka 2003;
- Mpango wa Utekelezaji wa Sera ya Sekta ya Ujenzi ya mwaka 2006.
- Mwongozo wa ununuzi unaohusisha utekelezaji wa miradi kwa njia ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2008;
- Rasimu ya Sera ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi ya mwaka 2008
- Mapitio ya Sera ya Sekta ya Ujenzi ya mwaka 2017.
Vyama na Bodi za Usajili
Baraza lilihamasisha uundwaji wa bodi za usajili na vyama vya wadau wa Sekta ya Ujenzi ;ikiwa ni pamoja na:
· Bodi
ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB);
· Bodi
ya Usajili wa Makandarasi (CRB);
· Bodi
ya Usajili wa Wahandisi (ERB);
· Chama
cha Wabunifu Majengo (AAT);
· Chama
cha Wahandisi Washauri (ACET);
· Chama
cha Makandarasi wa Ujenzi (TACECA);
· Chama
cha Barabara (TARA).
· Taasisi
ya Usuluhishi na Migogoro (TIArb);
· Taasisi
ya Wakadiriaji Majenzi (TIQS);
· Chama
cha Wajenzi wa Sekta isiyo Rasmi
(TAICO);
· Mfuko wa Maendeleo wa Sekta ya Ujenzi (CIDF);
Makongamano ya Sekta ya Ujenzi
Kuanzia mwaka 2001,Baraza limekuwa likiandaa makongamano ya sekta ya ujenzi kila baada ya miaka miwili. Madhumuni ya makongamano ya Sekta ya Ujenzi ni kusaidia upangaji, uratibu pamoja na kuboresha maendeleo ya Sekta ya Ujenzi kwa kuzingatia yafuatayo:
- Dira, malengo na mikakati ya maendeleo ya sekta ya ujenzi;
- Mikakati ya kukuza uwezo ili kuboresha utendaji katika sekta;
- Ukuaji wa sekta ili kukabiliana na ushindani wa Kimataifa;
- Uhusiano wa kimataifa.