Majukumu
Majukumu
Baraza ni kitovu cha uratibu wa sekta kwa taasisi zinazoshughulika na ujenzi ili kuleta umoja, uwiano na ushirikiano katika utendaji ndani ya sekta ya ujenzi. Hususani majukumu ya Baraza ni kama ifuatavyo:
- Kusimamia na kuongoza juhudi za kukuza na kuendeleza sekta ya ujenzi nchini Tanzania kwa kuzingatia ukuzaji wa uwezo wa ndani ya nchi ili kwenda sambamba na maendeleo na ushindani wa kimataifa;
- Kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayohusu sekta ya ujenzi na kutayarisha mapendekezo, maelekezo na utekelezaji wake;
- Kutoa ushauri wa kiufundi kwa wadau wa sekta ya ujenzi;
- Kukuza na kuratibu mafunzo bora kwa watu wanaojihusisha au watakaojihusishana sekta ya ujenzi;
- Kukuza, kuendesha na kuratibu utafiti katika masuala yanayohusiana na sekta ya ujenzi;
- Kutayarisha na kutunza orodha ya miradi na kuhamasisha utunzaji wa uenezaji wa taarifa zinazohusiana na sekta ya ujenzi;
- Kusimamia na kuratibu maendeleo na utekelezaji wa viwango, kanuni na miongozo ya kiufundi inayohusiana na sekta ya ujenzi;
- Kukuza na kuhimiza matumizi ya teknolojia za kisasa na utendaji endelevu,katika sekta ya ujenzi;
- Kukuza na kuanzisha makongamano yanayolenga katika ushirikiano na majadiliano katika masualayanayohusu sekta ya ujenzi;
- Kusimamia na kutathimini mwenendo wa utendaji wa sekta ya ujenzi;
- Kuanzisha na kusimamia mfuko wa fedha kwa ajili ya mafunzo ya wadau wasekta ya ujenzi;
- Kukuza na kusimamia ubora wa kazi za ujenzi ikijumuisha utoaji wa huduma ya ukaguzi wa kiufundi katika miradi ya ujenzi;
- Kuendeleza teknolojia za ujenzi unaolenga katika mbinu za utunzaji mazingira na kuzingatia afya na usalama;
- Kuendeleza utoaji huduma nje ya mipaka ya nchi kwa kuzingatia ubora katika sekta ya ujenzi;
- Kusimamia utatuzi wa migogoro katika sekta ya ujenzi.