Ukaguzi wa kiufundi

Madhumuni ya kufanya ukaguzi wa kiufundi katika miradi ya ujenzi ni kuwasaidia wawekezaji/watoa fedha kupata maelezo kuhusu mwenendo na utekelezaji wa miradi ikiwa ni pamoja na mapungufu yaliyopo,na utatuzi wake.

Ukaguzi unaweza kufanyika katika hatua yoyote ya mradi ikiwa ni pamoja na matayarisho ya utekelezaji, wakati wa utekelezaji na baada ya mradi kutekelezwa. Baraza limekuwa likitoa huduma hii kwa serikali na taasisi zake na sekta binafsi.

Kupitia Wizara ya Fedha, Baraza limekuwa likikagua miradi mikubwa inayogharamiwa na Serikali.