Utafiti
Kazi za utafiti zinazolenga katika kutambua matatizo mbalimbali na ufumbuzi wake yanayohusiana na sekta ya ujenzi kwa ujumla, ni mojawapo ya shughuli za Baraza. Tafiti zilizowahi kufanywa na Baraza ni pamoja na:
Tafiti kuhusu uanzishwaji wa mfuko maalum wa kuwasaidia wadau wa sekta ya ujenzi kupata mahali pa kukopa fedha au kupata dhamana kwa ajili ya miradi ya ujenzi;
Mahitaji ya rasilimali watu katika sekta ya ujenzi nchini Tanzania;
Mahitaji ya mafunzo kwa washauri na wakandarasi wa miundombinu ya umwagiliaji katika kilimo;
Uanzishwaji wa mfuko endelevu wa mafunzo kwa wadau wa sekta ya ujenzi nchini Tanzania;
Mapendekezo ya kuhuishwa sheria iliyoanzisha Baraza la Taifa la Ujenzi;
Utafiti kuhusu namna ya kuliwezesha kifedha, Baraza la Taifa la Ujenzi ili tuweze kutekeleza majukumu yake bila matatizo;
Utafiti kuhusu utendaji kazi katika miradi mikubwa ya ujenzi kwa kuzingatia ushiriki wa sekta ya umma na binafsi;
Utafiti kuhusu kitengo cha makontena bandarini;
Utafiti kuhusu wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi katika ujenzi.