Watazamaji wapendwa,
Karibuni kwenye Tovuti yetu ambayo inatoa maelezo na taarifa mbalimbali kuhusu sekta ya ujenzi nchini. Kama tunavyofahamu sote, tovuti hii ni mojawapo ya njia za mawasiliano za NCC kwa wadau pamoja na umma kwa ujumla.
Taarifa, takwimu, ripoti na nyaraka nyingine zinazowekwa hapa zinalenga kuwafahamisha kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea katika sekta ya ujenzi. Maoni na ushauri wenu ni muhimu sana kwetu kwani vitatusaidia kuboresha huduma tunazotoa kwa umma katika maendeleo ya sekta ya ujenzi.
Kupitia Tovuti hii, NCC itaendelea kutoa taarifa na habari kwa wakati ili kuhakikisha mnakuwa na uelewa sahihi na wa kina kuhusu shughuli za sekta hii.
Asanteni kwa kutembelea Tovuti yetu.