Wasifu
Asa Mwaipopo photo
Mha. Asa Mwaipopo
Mjumbe wa Bodi

Wasifu

Mhandisi Asa Mwaipopo ni Mshauri binafsi wa Sekta ya Madini na Mkurugenzi Asiye Mtendaji (Non-Executive Director) katika kampuni zinazojihusisha na uchimbaji madini, vifaa vizito vya migodi na ujenzi. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 35 katika sekta ya madini, akihudumu katika nafasi za kiufundi, uendeshaji, usimamizi na uongozi katika sekta za umma na binafsi. Aliwahi kuwa Mkaguzi wa Migodi Serikalini kabla ya kushika nyadhifa za juu za uongozi katika kampuni kubwa za madini, zikiwemo AngloGold Ashanti, African Barrick Gold (ABG), Mantra Tanzania na Acacia Mining.

Mhandisi Mwaipopo ana Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Uhandisi wa Madini kutoka Chuo Kikuu cha Zambia na Shahada ya Uzamili kutoka Camborne School of Mines, Chuo Kikuu cha Exeter, Uingereza. Ni Fellow na Rais wa sasa wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Mhandisi Mshauri aliyesajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB), Mwanachama wa Australasian Institute of Mining and Metallurgy (AusIMM), Mkurugenzi Aliyethibitishwa na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT), pamoja na Msuluhishi aliyethibitishwa na Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania (TIArb). Utaalamu na maslahi yake ya kitaaluma yanajikita katika uchambuzi wa uwekezaji, usimamizi wa ubora, utawala bora wa taasisi, na maendeleo endelevu ya sekta za madini na ujenzi.