Wasifu
Mercy G Jilala photo
Wakili. Mercy G Jilala
Mjumbe wa Bodi

Wasifu

Bi. Mercy Godlay Jilala ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika utawala wa sekta ya umma na uzingatiaji wa sheria za taasisi za umma. Kwa sasa ni Mkuu wa Huduma za Sheria katika Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB), ambapo anasimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na mifumo ya udhibiti wa taaluma ya uhandisi na maendeleo ya miundombinu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bi. Jilala ana uzoefu mpana unaojumuisha utumishi katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma, hali iliyomjengea umahiri katika masuala ya utawala bora, usimamizi wa vihatarishi, uendeshaji wa mashauri ya kisheria, majadiliano ya kisheria na uongozi wa kimkakati. Ni mwanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki (EALS), Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA), na Public Bar Association (PBA). Aidha, ameendelea kujiendeleza kitaaluma kupitia mafunzo mbalimbali ya uongozi ndani na nje ya nchi, na kwa sasa anaendelea na masomo ya Shahada ya Uzamivu (PhD kwa njia ya Tasnifu) katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.