Karibu
Mpendwa mtembeleaji
Karibu kwenye Tovuti yetu yenye taarifa na maelezo mbalimbali kuhusu sekta ya ujenzi nchini. Tovuti ni moja ya njia za mawasiliano zinazotumiwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kuwajuza wadau wake na umma mambo mbalimbali kuhusu Baraza na Sekta ya Ujenzi.
Taarifa zinanzotumiwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) zikiwemo takwimu, ripoti, na nyingine zinazo onekana kwenye tovuti hii zinalenga kukujuza yaliyomo, yanayojiri na yatakayojiri katika Sekta ya Ujenzi nchini hususan yanayohushu Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC). Tunaomba ushirikiano wako kwa kutupa maoni yako ili kuboresha huduma kwa umma kwa maendeleo ya Sekta na Taifa kwa ujumla.