Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) limebuni mfumo mpya wa uchakataji viwango vya bei za ujenzi na matengenezo ya barabara, lengo likiwa kuisaidia sekta ya ujenzi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Akiwasilisha mfumo wa uchakataji wa viwango vya bei za ujenzi na matengenezo ya barabara katika mkutano huo, Mha. Tumaini Lemunge wa NCC, amesema mfumo huo umetengenezwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi.
Mha. Lemunge amesema mfumo huo utaaidia taasisi, wahandisi washauri, na wakandarasi kufanya makadirio sahihi ya gharama.
“Mfumo huu utawasaidia watumiaji kuandaa makadirio ya gharama kwa miradi mbalimbali ya ujenzi na matengenezo ya barabara, pia utasaidia kulinganisha bei ya mzabuni na bei halisi ya soko, ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi unakuwa na tija,” amesema.
Ameongeza kuwa mfumo huo utapunguza changamoto ya utoaji wa bei zisizoendana na uhalisia wa gharama za miradi, jambo ambalo limekuwa likikwamisha utekelezaji bora wa miradi ya ujenzi.
“Natoa mwito kwa wakandarasi wote kuwasiliana na NCC ili waanze kutumia mfumo huu kwa ajili ya kupata bei halisi za zabuni, jambo ambalo litawasaidia kupanga kazi kwa ufanisi,” amesisitiza.
Gharama : Tsh
Hali : Completed
Ugharama :
Eneo / Mahali :
Muda :