Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) limetoa mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa vihatarishi (Risk Management) kwa wawakilishi wa idara zake, vitengo na sehemu ambao ni wahusika wa kubaini vihatarishi (Risk Champions) katika vitengo vyao, Pamoja na viongozi wao.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa NCC, Hannah Mwakalinga, mafunzo haya ya siku mbili yamelenga kuwapa uelewa na maarifa ‘risk champions’, viongozi wao, pamoja na watumishi wengine walioalikwa kuhudhuria mafunzo hayo ili waweze kuvitambua mapema vihatarishi vyovyote vilivyopo kwenye maeneo yao ya kazi na kazi zao.
“Umakini na matumizi mazuri ya muda katika mafunzo haya vitatufanya tupate kile tunachokikusudia, kwa faida ya taasisi yetu. Kadhalika maarifa na uelewa mpana tunaoupata tufaidishe na wengine kwa kuwafundisha,”Mwakalinga amesema.
Muwezeshaji wa mafunzo haya ni Mkaguzi wa Ndani Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha (MoF)-ACGEN, Bariki Mtunha. Mafunzo haya yamefanyika katika ofisi za NCC zilizopo ghorofa ya chini kwenye jengo la Mfuko wa Barabara.
NCC inatoa huduma zifuatazo; mafunzo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi, huduma za ushauri wa kiufundi, usuluhishi wa migogoro, ukaguzi wa kiufundi, utafiti na machapisho, miongozo mbalimbali ya sekta ya ujenzi na taarifa za masuala tofauti yahusuyo sekta hiyo ya ujenzi.