Salamu za Pongezi kwa Mhandisi, Dk Leonard Chamuhiro-Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

News Image Dec, 15 2020

BODI ya Wakurugenzi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), Menejimenti na Wafanyakazi wote wa baraza hili, tunayofuraha kukupongeza Injinia, Dk. Leonard Chamuhiro kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi. Hongera sana.

Sisi wana familia ya NCC, tunaamini kuwa Rais John Pombe Magufuli aliona uwezo wako na shauku yako ya kuiletea nchi maendeleo hasa kupitia sekta ya ujenzi na uchukuzi, ndio maana akakupa nafasi hiyo. Ameamini unaweza, nasi tunaamini kuwa unaweza. Pokea pongezi zetu nyingi na Mungu akuongoze katika utendaji wako.

Tukiwa wadau wako katika sekta ya Ujenzi, tunakuahidi ushirikiano wa hali ya juu, ili uweze kufanikisha majukumu yako, kama inavyokusudiwa. Mwenyezi Mungu akuongoze katika hii safari yako.