Changamoto sekta ya ujenzi kupata ufumbuzi Leo.

News Image Jan, 15 2018

Baraza la Taifa la ujenzi limekutana na wadau wa sekta ya ujenzi kujadili fursa mbalimbali pamoja na changamoto zilizopo katika sekta ya ujenzi kwa lengo la kuimarika na kuendelea kuzidi kujenga uchumi wa nchi hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inajikita katika uchumi wa Viwanda.

Hayo yamesemwa na mtendaji mkuu wa baraza la Taifa la ujenzi Mhandisi Matiko Samson Mturi ambapo amesema katika mkutano huu umewahusisha

wakandarasi,watengenezaji wa vifaa vya ujenzi ,wasambazaji wa vifaa, watu wa Bima,Wizara ya ujenzi, vyama vya kutetea wakandarasi,ewura,wabunifu majengo na wadau mbalimbali wa ujenzi wakiwa na lengo moja la kuwasikiliza wote hao changamoto wanazokabiliana Nazo ili wazipatie ufumbuzi kuboresha zaidi sekta ya ujenzi kuleta tija katika nchi.

Akizianisha baadhi ya changamoto mbalimbali zinazowabili ni pamoja na ukosefu wa uzoefu wa ujenzi wa miradi mikubwa kama wa reli wa standard Gauge unahitaji uzoefu mkubwa hivyo kupitia changamoto hiyo wataangalia namna gani serikali itawasaidia katika kuwawezesha kupata ujuzi zaidi kupitia wahandisi wakigeni wanaokuja kutekeleza miradi hiyo wanawapatia mafunzo.

Naye mkurugenzi wa Sera na mipango Wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano mhandisi Elizabeth Taghora amesema katika mkutano wa Leo kutapatikana ufumbuzi wa kila changamoto zilizopo katika sekta ya ujenzi na kuhakikisha sekta ya ujenzi inaimarishika na inazidi kuchangia uchumi wa nchi kwa kuwa sekta ya ujenzi ni miongoni mwa sekta zinazotegemewa nchini hasa katika harakati za Sasa za kuelekea uchumi wa viwanda na ndio maana wadau wote wa sekta ya ujenzi wamekutana kujadili changamoto mbalimbali na kuzipatia ufumbuzi wenye tija.

Vile vile katibu wa chama cha makandatasi wa barabara Magret Ngianaeli amesema wamesema kupitia mkutano wa leo wa majadiliano watahakikisha wanatoka na Sera ambayo itawapa usawa makandarasi wazawa na kipaumbele zaidi ili wazidi kusikika na kupata fursa zaidi za kazi na uzoefu.