NCC kutoa mafunzo ya usimamizi wa mikataba ya ujenzi

News Image Sep, 27 2022

BARAZA la Taifa la Ujenzi (NCC) limeandaa mafunzo ya siku tano ya usimamizi bora wa mikataba ya ujenzi kwa ajili ya watu wa fani mbalimbali nchini, watakaopenda kupanua uelewa wao juu ya mikataba ya ujenzi kwa manufaa yao, taasisi zao na hata taifa.

Mafunzo hayo yataendeshwa na wabobezi wenye kuaminiwa katika masuala ya usimamizi wa mikataba ya ujenzi kuanzia Oktoba 17 hadi 21, mwaka huu, katika Hoteli ya Benaco jijini Mbeya.

Kulingana na umuhimu wa mafunzo hayo, Baraza la Taifa la Ujenzi kuanzia leo, linakaribisha maombi ya kujiunga na mafunzo hayo yatakayojumuisha vipengele kadha wa kadha vinavyohusu masuala hayo ya usimamizi wa mikataba ya ujenzi mikataba.

Ada kwa mshiriki mmoja ni Shilingi 750,000/= pekee, itakayotumika kugharamia huduma mbalimbali zitakazotolewa wakati wote wa mafunzo hayo, yaani katika siku zote tano, ambazo ni pamoja na chai wakati wa asubuhi, chakula cha mchana, chai ya jioni na notisi za mambo yatakayofundishwa .

aidha, fedha hizo pia zitatumika kugaramia huduma mbalimbali nyingine kama vile ukumbi utakaotumika kufanyia mafunzo hayo na malipo ya wakufunzi.

Kwa mujibu wa muandaaji msimamizi wa mafunzo, ambaye ni Mkadiriaji Majenzi (QS) Anitha Mallewo anasema, "Tumeanza kupokea maombi ya ushiriki katika mafunzo hayo na tungependa wanaotaka kushiriki wakahihishe wanafanya 'booking' mapema na kulipa ada hadi kufikia Oktoba 10, mwaka huu,".

Anasema anayehitaji maelekezo zaidi anaweza kupiga simu za ofisi zinazoonekana kwenye tangazo la kozi au kumpigia moja kwa moja kwa namba za mkononi 0687242759.

Anasisitiza kuwa malipo yanafanywa katika akaunti ya benki ya NMB inayomilikiwa na NCC kupitia namba za kumbukumbu zinazotolewa na wahasibu wa Baraza la Taifa la Ujenzi.