Kujiunga na Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG)

Baraza la Taifa la Ujenzi linapenda kuwataarifu wateja wake, wadau wa ujenzi na Umma kwa ujumla kwamba kuanzia tarehe 15/04/2019 malipo yote ambayo yatafanyika Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) yanatakiwa kufanyika kwa kutumia Namba ya Malipo (Control Number).

Hivyo, mteja anatakiwa kuja au kuwasiliana na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) kwa ajili ya kupatiwa Namba ya Malipo (Control Number) kwa ajili ya kufanya malipo Benki au kupitia simu ya mkononi.

Malipo yatakayofanywa bila ya Namba ya Malipo (Control Number) hayatapokelewa

Tunashukuru kwa ushirikiano wako.

Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC)